BURUDANI
Video:Dayna Nyange adai mastaa wengi hawajui kutongoza ‘wananitongoza lakini hawanishawishi’
Msanii wa muziki Dayna Nyange ambaye pia ni mama wa mtoto mmoja, amefunguka na kuzungumzia kiundani kauli yake ambayo amekuwa akitoa kila mara kwamba hawezi kutoka kimapenzi na mastaa
wenzake.Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Komela’ akiwa amemshirikisha Billnass, amedai anatongozwa na mastaa wengi lakini wanashindwa kumshawishi.
“Sijawahi kudate na staa na si kwamba wakaka wazuri hawapo, na sio kwamba hawanitokei, labda hawajui kutongoza vizuri,” alisema Dayna. “Kwa sababu sijawahi kushawishika kutembea na staa na sipendi kutembea na staa, so wakati mwingine unaweza ukawa haupendi kitu lakini ukashawika kuingia lakini mimi bado hajatokea,”
Katika hatua nyingine muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwajili ya kazi mpya pamoja na kolabo za kimataifa ambazo hakuziweka wazi.
0 comments