Breaking News
Loading...

NEWS: MTANDAO WA WANAFUNZI WAKAMILISHA KUJINOA KUPINGA MALIPO YA 15% YA MKOPO MAHAKAMANI

Share on Google Plus


TAARIFA KUTOKA KWA LHRC na TSNP 

LHRC na TSNP tumekutana leo kujadili suala la malipo ya 15% kwa watanzania waliokopeshwa na bodi ya mikopo. 

Tumefanya majumuisho ya hoja za kisheria kwa wajumbe waliofika kikaoni na wale ambao wamewasilisha maoni yao kwa njia ya simu, barua pepe na jumbe za kawaida kutoka kila kona ya Tanzania. Njia ya kushinda dhahama hii ni pana sana.

Muhimu zaidi, tunashukuru tumepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wanafunzi na kutoka kwa vyama mbalimbali vya wafanyakazi wanaokiri kuonja uchungu mzigo huo mzito. Wengi wanasema wako tayari kulipa 8% kama sehemu ya deni lao ila sio 15% kwani ni kiwango kikubwa sana.

Hata hivyo, matamanio yetu ni kuona vyama vingine vya wafanyakazi nchini vinachukua hatua ya kuunga juhudi hizi kama ambavyo TUCTA wamefanya hii leo.

 Wanachama wao wanatoa sehemu ya misharaha yao kwajili ya mambo kama haya yanayogusa maisha yao moja kwa moja, sio kwajili ya viongozi na watumishi wengine kujilipa mishahara na posho.

Pamoja na dalili zote kuonesha ushindi, imani yetu kama taasisi (TSNP) ni kupambana kukataa mzigo huu(15%) mzito mpaka tuone ushindi. Tutashinda. 15% haikubaliki.

©Bob Wangwe
-Mkurugenzi wa sheria TSNP

You Might Also Like

0 comments

About me

Like us on Facebook

MICHEZO

Blog Archive