BURUDANI
MREMBO TUNDA AZUA UTATA KWENYE BATA ZAKE
Muuza nyago kwenye video za mastaa wa Bongo Fleva, Tunda Sebastian ambaye wiki chache zilizopita alikumbwa na msala baada ya kuitwa kuhojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi ‘Sentro’ kwa wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amefunguka kuwa, licha ya kukumbwa na sekeseke hilo, hawezi kuacha maisha ya kula bata.
Akipiga stori na Over Ze Weekend baada ya kuulizwa kama amebadili mfumo wa maisha aliyokuwa nayo mwanzo ya kuonekana akijiachia kwenye mahoteli makubwa, Tunda alisema kuwa hayo ndiyo maisha aliyochagua kuishi na kamwe hawezi kubadilika.
“Hayo mambo ya bata ndiyo maisha yangu, siwezi kuacha na wala hayaingiliani na msala nilioupata kwani uzuri situmii pombe. Hata kwenye mambo ya mavazi ndiyo mfumo wa maisha yangu, siwezi kusema kuwa nitaacha kuvaa hivi, bali nitabadilika kuendana na mazingira,” alisema Tunda
ACHA COMMENT YAKO HAPA
ACHA COMMENT YAKO HAPA
0 comments