MANJI KATIKA TUHUMA NYINGINE ZA UHAMIAJI
DAR ES SALAAM:
Masahibu mengi bado yanatajwa kumuandama Mfanyabiashara YUSUPH MANJI baada ya Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam siku ya tarehe 14 Feb, 2017, kumtaka mfanyabiashara huyo maarufu na mmiliki wa Quality Plaza, Yusufu Manji kuripoti uhamiaji mara baada ya kutoka hospitali alikolazwa.
Ofisa Uhamiaji wa mkoa huo, John Msumule akizungumza na wanahabari leo.
Ofisa Uhamiaji wa mkoa huo, John Msumule ametoa taarifa hiyo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema Manji anatakiwa kufanya hivyo kwa kudaiwa kuwa ameajiri watu wanaoishi nchini na kufanya kazi kinyume cha sheria.
Ofisa akionesha paspoti hizo.
“Siku ya Ijumaa tulifanya upekuzi kwenye Jengo la Quality Plaza (linalomilikiwa na Yusuf Manji, lililopo Barabara ya Airport), tukakamata paspoti 126 ambapo paspoti 25 ndizo zina makosa, wamiliki wake hawana vibali na wanafanya kazi kinyume na utaratibu, watapelekwa mahakamani pamoja na mwajiri wao, Yusuf Manji ili akajibu mashtaka hayo.
“Ilikuwa tumkamate jana lakini tukasikia kwamba amelazwa hospitali… hivyo akitoka hospitalini awasili haraka ofisi hii ili tumuunganishe kwenye kesi ya kuwaajiri watu wasio na vibali….”Alisema Msumule.
Manji alishikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alhamisi iliyopita baada ya kutajwa na Mkuu wa Mkoa huo, RC Makonda kuwa anatakakiwa kuripoti Sentro kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu tuhuma za madawa ya kulevya.
Endelea kufuatilia Akisi Tv kila siku
0 comments