BURUDANI
Jay Z kuzindua mradi wake mpya wa mfuko wa fedha
Usilete mchezo na Jay Z kwenye suala la kutafuta fedha. Rapper huyo ambaye anakadiriwa kuwa na utajiri wa dola milioni 610 amepanga kufungua mfuko wa mradi wa fedha.
Kwa mujibu wa mtandao wa Axios Jay Brown ambaye ni mtu wa karibu wa rapper huyo atakuwa ni mmoja kati ya watu ambao watakaohusika katika mradi huo.
Mpaka sasa Jay Z ameshawekeza kwenye miradi mbalimbali na mikubwa duniani ikiwemo kwenye kampuni ya usafirishaji kwa njia ya mtandaoni (Uber) ambapo inadaiwa kwa mwaka 2011 ambapo aliwekeza kampuni hiyo ilikuwa na thamani ya dola milioni 300 lakini kampuni hiyo sasa ina thamani ya takribani dola bilioni 62.5.
Kampuni nyingine ambayo amewekedha fedha nyingi ni Stance pamoja na mtanda wa Tidal ambao unamilikiwa na baadhi ya wasanii wakubwa wa Marekani pamoja na kampuni ya Sprint ambayo imepewa hisa asilimia 33.
0 comments