Breaking News
Loading...

TUNATAKA RAIS AONGEZEWE MUDA MADARAKANI- BUNGE LA MISRI

Share on Google Plus

Wawakilishi wa Bunge la Misri wamesema kuwa, wanataka kipindi cha uongozi wa Rais wa nchi hiyo kiongezwe.

Ismail Nasserddin, mmoja wa Wabunge wa Misri amesema kuwa, wawakilishi wa Bunge la nchi hiyo wanafanya juhudi za kuongezwa kipindi cha uongozi wa Rais kutoka miaka minne na kuwa mika sita.
Wabunge hao wanasema kuwa, muda wa sasa wa uongozi wa Rais hautoshi kwa kiongozi huyo wa nchi kutekeleza mipango yake.
Aidha Mbunge huyo wa Misri amesema, hivi sasa kunafanyika juhudi pia katika Bunge hilo kwa ajili ya kubadilisha mfumo wa utawala wa nchi hiyo sambamba na kumpatia mamlaka zaidi Rais wa nchi. Taarifa zaidi kutoka nchini Misri zinasema kuwa, tayari Wabunge wanaounga mkono mpango huo wameanza kukusanya saini zao.
Bunge la Misri ambalo uchaguzi wake ulifanyika baada ya Rais Abdel Fattah al-Sisi kuingia madarakani, linaiunga mkono serikali ya jenerali huyo wa kijeshi ambaye anatuhumiwa kuindoa madarakani serikali ya Rais halali Muhammad Muhammad Mursi ambaye ndiye rais kwa kwanza wa nchi hiyo kuchaguliwa kwa njia ya kidemokrasia.
Kwa sasa serikali ya Misri inakabiliwa na tatizo kubwa la uchumi. Moja ya sababu kuu zilizosababisha kutokea matatizo ya kiuchumi nchini humo ni machafuko na ukosefu wa usalama katika maeneo tofauti ya nchi hiyo.
SOURCE : RADIO TEHRAN
ACHA COMMENT YAKO HAPA

You Might Also Like

0 comments

About me

Like us on Facebook

MICHEZO

Blog Archive