KIMATAIFA
MAUAJI YA KUTISHA HAIJAWAHI KUTOKEA DUNIANI
Hivi sasa kuna uvumi kwamba kifo cha Kim Jong nam -ndugu wa kambo wa rais wa Korea kaskazini Kim Jong Un huenda pia aliuawa.
Iwapo hilo limethibitishwa kuwa kweli, basi uvumi umezuka kwamba wanawake wawili waliomuwekea kitambaa cha kujifutia chenye sumu katika mdomo wake alipokuwa akitembea katika uwanja wa ndege mauaji yake yanaorodhshwa miongoni mwa watu wachache waliouawa kupitia njia zisizo za kawaida
Chai ya sumu ya Polonium
Kifo cha Alexander Litvinenko's kinadaiwa kuwa cha mtu maarufu katika miaka ya hivi karibuni.
Jasusi huyo wa Urusi alianza kuugua mnamo tarehe 1 mwezi Novemba 2006, saa chache tu baada ya kunywa chai katika hoteli ya Millenium huko Mayfair pamoja na majasusi wenzake wawili.
Baada ya kifo chake majasusi hao ndio waliokuwa washukiwa wakuu katika kifo chake.
Wakati bwana Litvinenko alipolazwa hospitalini mnamo tarehe 3 mwezi Novemba aliwaambia madaktari amepewa sumu.
Baadaye, alimtaja rais Vladmir Putin akisema ''ndiye aliyesababisha kifo chake''.
Wakati huohuo nywele zake zilianza kuanguka huku viungo vyake vya mwilini vikishindwa kufanya kazi-huku madaktari katika hosptali ya chuo kikuu cha London nchini Uingereza wakishindwa kupata chanzo.
Baadaye ilibainika ni nini kilichomuua kwani wanasayansi bingwa wa Uingereza wanaofanya utafiti wa zana za nyuklia huko Aldermaston walifanikiwa kugundua kwamba tembe ya polonium 210 iliotumika katika bomu la kwanza la nyuklia ndio chanzo cha mauaji hayo.
Hakuna kitu madaktari walichoweza kufanya
Bwana Litvinenko aliambia BBC Urusi kwamba alikuwa akichunguza mauaji ya mwanahabari Anna Politkovskaya mwezi uliopita wakati aliposhambuliwa, Alifariki tarehe 23 mwezi Novemba.
Mwavuli uliowekwa sumu.
Raia wa Bulgaria Georgi Markov alikuwa akisubiri kupanda basi mnamo tarehe 7 mwezi Septemba wakati alipohisi amedungwa kisu katika paja lake.
Bwana Markov mwenye umri wa miaka 49 aliangalia nyuma na kumuona mtu ambaye alikuwa amebeba mwavuli akikimbia na kupanda teksi.
Ni baadaye alipokamilisha kazi yake ya huduma ya BBC nchini Bulgaria aliporudi nyumbani na kuanza kuugua.
Bwana Markov ambaye alikuwa mpinzani wa serikali ya kikomyunisti ya Bulgaria alifariki miaka minne baadaye.
Maafisa baadaye waligundua kwamba aliwekewa sumu ya ricin ambayo ilidaiwa kutiwa katika mwavuli huo.
Hakuna mtu aliyeshtakiwa kwa mauaji yake ikiwa ni mabaya zaidi katika vita baridi, lakini Bwana Markov alisema kuwa anaamini kwamba majasusi wa Urusi KGB walihusika katika shambulio lake.
Dubu aliyebeba shoka.
Jörg Jenatsch alikuwa muhubiri ambaye alibadilika na kuwa mwanasiasa maarufu katika vita vya miaka 30 nchini Switzerland.
Lakini licha ya mafanikio yake yote ni kifo chake mwaka 1639 katika nyumba moja ya kulala huko Chur ambacho kitakumbukwa sana.
Bwana Jenatsch, ambaye alikuwa amesifika kwa huduma yake alikuwa katika sherehe wakati kundi moja la watu lilipowasili na kutaka kujiunga nao.
Kiongozi wa kundi hilo alikuwa amevaa kama dubu.
Kundi hilo liliruhusiwa kuingia na dubu huyo ambaye utambulisho wake haukujulikana kabla ya kumkata bwana Jenatsch hadi kufa kwa kutumia shoka.
Inadaiwa kuwa shoka lililotumiwa ndio hilo hilo alilotumia kumuua mpinzani wake.
Chuma cha moto
Zaidi ya miaka 700 huenda imepita tangu mfalme Edward wa pili alipouawa kati mji wa Gloucestershire, lakini bado tunaweza kukumbuka.
Tunachojua ni kwamba mfalme Edward wa pili alikamatwa na kulazimishwa kuwachia ufalme kwa niaba ya mwanawe ambaye alikuwa Edward wa tatu baada ya mkewe Isabella na mpenziwe Roger Mortimer kuvamia Uingereza mwaka 1326.
Edward wa pili baadaye alifungiwa huko Berkeley ambapo alifariki mwaka uliofuatia.
Lakini kulingana na habari zilizopitishwa kutoka kizazi kimoja hadi chengine hakufariki usingizini kama ilivyodaiwa.
Badala yake, habari zinasema kuwa alitiwa chuma cha moto katika tupu yake ya nyuma na hivyobasi kuchoma viungo vyake vya mwili bila kuwacha alama yoyote.
Habari hiyo huenda ilipingwa kuwa uvumi na wanahistoria wengi katika miaka iliofuata, lakini hatua hiyo haijawazuia wengine kuendelea kusambaza habari hiyo.
Mara nyengine hata mipango iliopangwa vizuri inaweza kuharibika.
Na kuna wakati ambapo pia chombo cha usaidizi wakati mpango huo unapofeli kinaweza kufeli. Iwapo hilo linaaminika linaweza kutokea basi hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa watu waliopanga njama za kifo cha Grigory Rasputin 1916.
Inaonekana kuwa watu wachache hawakumpendelea mkulima huyo aliyependwa sana na kuamua kumuua. Lakini baada ya kumpeleka hadi katika jumba la mwanamfalme Felix Yusupov huko St Petersburg mambo yalianza kwenda mrama.
Wauaji wake ,mwanamfalme Yusupov na Vladimir Purishkevich, ambaye alikuwa mbunge kwanza walimlisha keki iliokuwa na sumu. Keki hiyo haikumuathiri na hivyobasi wauaji hao wakaamua kutumia bunduki zao. Risasi walizotumia zilishindwa kumuangusha na ngumi zao katika kichwa chake pia hazikufaulu.
Iwapo wauaji wake wanafaa kuaminiwa ilichukua risasi nyengine nne kufanikiwa kumuua Rasputin, ijapokuwa uvumi mwengine unasema kuwa walilazimika kumzamisha majini.
Lakini madaktari waliochunguza kifo chake wanasema kuwa alipigwa risasi moja katika tumbo na hivyobasi kupoteza damu nyingi.
0 comments