KIMATAIFA
BREAKING: RAIS AMTUMBUA NA KUMTIMUA KAZI MKUU WA MAJESHI
Rais wa Gambia Adama Barrow amemuachisha kazi mkuu wa majeshi wa nchi hiyo Ousman Badjie.
Hatua hiyo ya Rais Barrow imekuja kutokana na Badjie kutangaza mwezi Disemba mwaka jana baada ya uchaguzi mkuu kuwa atafuata amri ya Rais aliyepita Yahya Jammeh ambaye alishindwa katika uchaguzi huo.
Hata hivyo wanajeshi wa Gambia hawakuweza kutii amri kutoka kwa mkuu huyo wa majeshi ambaye alikuwa chini ya Jammeh ambaye baada ya muda alikubali kuachia madaraka hayo na kukimbilia nchini Equatorial Guinea.
Na sasa Masanneh Kinteh ambaye aliwahi kufanya kazi nchini Cuba anachukua nafasi hiyo ya Badjie. Baada ya kuteuliwa katika nafasi hiyo, Kinteh alitaja jambo lake la kwanza ambalo atalifanya katika jeshi lake ni kuwafaja wajiamini ili waongeze hamasa yao.
“My immediate priority as chief of defence staff is to bring back the confidence in the troops to lift their morale,” amesema Kinteh.
0 comments