BURUDANI
Hiki ni kitu ambacho Amber Lulu hawezi kufanya na Gigy Money kwa sasa
Hakuna mtu hapa Bongo ambaye hakumbuki urafiki wa warembo wauza nyago(Video Vixens)Amber Lulu na Gigy Money, waliokuwa karibu na vitu vingi walifanya pamoja.
Mwaka jana,urafiki wao ulivunjika baada ya Amber Lulu kusemekana kwamba alikamatwa na madawa ya kulevya huko Arusha,na Gigy Money akawa anamuua Shosti yake huyo kwenye vyombo vya habari.
Umepita muda sasa tangu kila mmoja achukue time yake, lakini time hii wamekutana kwenye fani nyingine tena. Gigy Money aliingia kwenye muziki mwaka jana,na Amber Lulu naye ameenda huko huko kwa kutoa pia ngoma yake.
Kwenye interview na Kipindi cha Supermega cha Kings Fm kinachoongozwa na Prince Ramalove, Amber lulu amedai kuwa japo wamekutana kwenye fani hii ya muziki tena,lakini hawezi kufanya collabo na rafiki yake huyo wa zamani.
“Am not ready,” amesema Lulu. “Nahisi kuna vitu vinatofautiana. Anachofanya yeye na ninachofanya mimi ni vitu viwili tofauti, kwahiyo sidhani kama inaweza ikatokea labda hapo baadaye sana,ila sio sasa hivi,” ameongeza.
Katika hatua nyingine mrembo huyo amewaomba mashabiki wake na wapenzi wa muziki mzuri waendelee kumsapoti kwenye ngoma yake hiyo ambayo kichupa chake kinapatikana Youtube tayari.
0 comments