BURUDANI
Luis Munana Afichua Siri Nzito ya Mapenzi Aliyonayo kwa Wema Sepetu.
Wiki iliyopita picha za mtandaoni zilionesha kuwa Wema Sepetu na mshiriki wa
Big Brother Hotshots kutoka Namibia, Luis Munana wamefunga ndoa.
Hakuna taarifa rasmi kutoka kwa wawili hao baada ya ‘ndoa’ hiyo kufungwa
lakini Luis ameimbia Clouds E ya Clouds FM kuwa picha zilizosambaa na
halisi na zilipigwa kwenye tukio hilo lililoshuhudiwa na familia zao zote mbili.
“Kwa sasa siwezi kuzungumzia chochote kuhusu picha hizo na ndio maana
niliamua kuzifuta kwenye akaunti yangu kwakuwa lilikuwa tukio la faragha,” alisema Luis.
Luis alisema alikutana na Wema kwenye Instagram Party na kubaini kuwa wote
walikuwa wakipendana bila kujua. “Alikuwa crush wangu, nami nilikuwa crush wake,” alisema.
STORY TAMMMM....
0 comments