BURUDANI
Marry You ya Diamond yaingia kwenye Top 20 za Vevo Marekani
Diamond Platnumz anazidi kufikia malengo aliyojiwekea mwaka huu. Video ya wimbo wake, Marry You aliyomshirikisha Ne-Yo, imeingia kwenye Top 20 za Vevo nchini Marekani. Chati hiyo inahusisha wasanii wapya wa Marekani.
Video hiyo sasa inapigana vikumbo na ngoma za rappers maarufu wakiwemo Desiigner na Lil Yatchy. “Kwahiyo @vevo ndio wameamua iwe hivyo? Top 20 New Artists Videos in the U.S na #MarryYou imo? Kwanini wanafanya upendeleo?,” ameandika meneja wake, Sallam.
0 comments