Breaking News
Loading...

MANJI KUPANDISHWA KIZIMBANI LEO

Share on Google Plus

Habari zilizotufikia zinaeleza kwamba, mfanyabiashara mkubwa na mmiliki wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji anatarajiwa kupandishwa kizimbani leo.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, Manji atapandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, ikiwa ni siku kadhaa baada ya mfanyabiashara huyo kushikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central), alikoenda kuitikia wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Jumatano ya wiki iliyopita, Makonda alitangaza majina ya watu aliosema wanadaiwa kujihusisha na biashara na matumizi ya madawa ya kulevya na kuwataka waripoti Sentro Ijumaa iliyopita.

Hata hivyo, Manji aliripoti Alhamisi na kuanzia siku hiyo, ameendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano ambapo Jumapili iliyopita, hali yake ilibadilika ghafla na kukimbizwa Hospitali ya Muhimbili, ambako Jumatano hii amefanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, iliyo ndani ya Hospitali ya Muhimbili.

Habari zaidi zitaendelea kukujia kupitia hapahapa, endelea kufuatilia mtandao huu.

You Might Also Like

0 comments

About me

Like us on Facebook

MICHEZO

Blog Archive