BURUDANI
JOSE MOURINHO AMLILIA kocha Claudio Ranieri wa Leicester City
Kocha wa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Leicester City, Claudio Ranieri ametimuliwa kwenye klabu hiyo.
Leicester iko katika nafasi ya 17, na ikipoteza alama moja tu itakuwa kwenye mstari wa kushuka daraja.
Kutimuliwa kwa kocha huyo kumekuja saa 24 baada ya kichapo cha magoli 2-1 walichopata kutoka kwa FC Seville.
Leicester City msimu uliopita ilitwaa ubingwa kwa zaidi ya alama 10 mbele, lakini msimu huu, mpaka sasa wamecheza michezo 25 ya ligi na kushinda mitano pekee, na imesalia michezo 13 ligi kuisha.
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ametoa kauli kuhusu kufukuzwa kwa kocha huyo huku akimpongeza kwa historia aliyoiweka katika ligi hiyo.
“CHAMPION OF ENGLAND and FIFA MANAGER of THE YEAR.sacked. Thats the new football claudio.keep smiling AMICO.nobody can delete the history you wrote.,” aliandika Jose kupitia Instagram.
0 comments