BURUDANI
Fid Q afunguka urafiki wake na AY ulipotoka, amtaja aliyemkutanisha naye
Fid Q amefunguka kuhusu urafiki wake na AY pamoja na mtu ambaye amewaunganisha.
Rapper huyo amedai kuwa urafiki wao umekuwa ni wa muda mrefu zaidi japo watu wengi hawafahamu hilo na aliyewakutanisha ni meneja wake wa zamani ambaye pia alikuwa anatengeneza video, David Latta.
“Yule bwana hajawahi kunifahamu kama mimi kuwa Fid Q wala mimi sijamfahamu yeye kuwa AY, tunafahamiana long time lakini ni kitu ambacho watu wamekuwa hawajui. AY kanifahamu mimi kwenye kufuatilia magazeti kama Msanii Afrika yale, kusikiliza redio Free Africa akajua kuna Fid Q Mwanza ananijua huko,” amesema Fid.
“Nafanikiwa kupata video yake ya kwanza ya ‘Raha Tu’, aliyemfanyia ni David Latta ambaye alikuwa ni meneja wangu mimi. Kwahiyo tuna stori zetu nyingi ambazo zinatuunganisha tunakuwa washkaji vile,” ameongeza.
0 comments