KIMATAIFA
HATARI: TRUMP KULIONGEZEA 'MINOFU' NA 'MASHAVU' JESHI LAKE KWA DOLA BILLION 54'
Maafisa wa ikulu ya White House wanasema kuwa bajeti ya ulinzi nchini Marekani itaongezeka kwa dola bilioni 54, ikiwa ni karibu asilimia 10.
Fedha hizo zitapatikana kwa kupunguza bajeti za programu zisizo za kijeshi, ikiwemo misaada ya kigeni na fedha zinazotumiwa kwa utunzi wa mazingira.
Mipango hiyo itawasilishwa kwa bunge la Congress mwezi ujao.
Wakati huo huo idara ya ulinzi imewasilisha kwa White House, mipango ya kulishinda kundi la Islamic State ambayo Rais Trump alikuwa ameitaka idara hiyo kuishughulikia.
BBC
0 comments