Breaking News
Loading...

China yasitisha ununuzi wa makaa kutoka Korea Kaskazini

Share on Google Plus

Uchina imetangaza kuwa inasitisha kwa muda ununuzi wa makaa kutoka Korea Kaskazini, katika juhudi za kuzidi kuichagiza Korea Kaskazini, baada ya jaribio la kombora la karibuni kabisa kufanywa na Korea Kaskazini.
Makaa ni bidhaa muhimu kabisa inayosafirishwa na Korea Kaskazini, na shehena za makaa zinazopelekwa Uchina, ndizo zinazobeba uchumi wa uchumi tete wa Korea Kaskazini, na pengine zinaleta sarafu ya kigeni, inayogharamia mradi ya silaha za nuklia za nchi hiyo.
Mwaka jana, wakuu wa Uchina walisema watasimamisha ununuzi wa makaa kutoka nchi hiyo, na kuruhusu tu kwa maslahi ya ustawi wa raia wa Korea Kaskazini.
Hata hivyo data ya Uchina inaonesha, Korea Kaskazini imeiuzia Uchina makaa asilimia 12 zaidi mwaka jana.

You Might Also Like

0 comments

About me

Like us on Facebook

MICHEZO

Blog Archive