Breaking News
Loading...

Genevieve (Miss TZ 2010): Ningepata nafasi ya kushiriki tena Miss Tanzania ningeshiriki

Share on Google Plus

 Wakati baadhi ya washindi wa shindano la Miss Tanzania wakiwa hawatamani tena kurudi katika shindano hilo linapomalizika endapo watapata nafasi nyingine lakini ni tofauti kwa Miss Tanzania 2010, Genevieve Mpangala ambaye amedai anatamani kushiriki tena kama angepata nafasi hiyo.

Akiongea na Bongo5, mrembo huyo amesema, “Hata mara moja, I will definitely do it again kabisa, na
 hivi kwa sababu nilishafika I saw yaani I will have a fresher mind, nisingeweza kusita kama ningepata nafasi ya kushiriki tena.”
Genevieve ameongeza pia kwa kutaja vitu ambavyo anapenda katika maisha yake, amesema, “Mimi ni mpenzi wa kusafiri, napenda kujifunza vitu vipya. Napenda kuona vitu vipya napenda kujaribu vyakula vipya.”
Kwa sasa mrembo huyo anaimba muziki wa Bongo Fleva na tayari ameshaachia wimbo wake wa kwanza ‘Nana’ ambao umetayarishwa na Luffa.

You Might Also Like

0 comments

About me

Like us on Facebook

MICHEZO

Blog Archive