KIMATAIFA
MSIKITI mwingine wachomwa moto Marekani, matamshi ya KIBAGUZI ya TRUMP yanaendela kufanya kazi
Kundi la waokoaji katika mji wa Hillsboro kwenye jimbo la Florida nchini Marekani wametangaza kuwa Msikiti na Kituo cha Kiislamu cha New Tampa cha mji huo kimechomeka kwa moto na kwamba ushahidi unaonesha uhalifu huo umefanyika kwa makusudi.
Ripoti zinasema, wakati wa kutokea moto huo hakuna mtu aliyekuwemo ndani ya msikiti huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Mahusiano ya Marekani na Uislamu (CAIR) huko - Florida, Hassan Shibly, amesema moto huo ni kitendo cha ugaidi na amemtaka Rais wa Marekani Donald Trump akiri na kukubali uhakika huo.
Takwimu zinaonesha kuwa uhalifu unaosababishwa na chuki hususan dhidi ya Waislamu umeongezeka nchini Marekani tangu Donald Trump achaguliwe kuongoza nchi hiyo.
Wakati wa kampeni zake za uchaguzi, Trump alitangaza kuwa endapo atashinda uchaguzi wa rais atawazuia Waislamu kuingia Marekani na kujenga ukuta katika mpaka wa nchi hiyo na Mexico ili kuzuia wahamiaji kuingia Marekani.
Wataamu wanasisitiza kuwa, matamshi ya kibaguzi kama hayo ya Donald Trump yanachochea sana mashambulizi na hujuma zinazofanywa na makundi ya kibaguzi dhidi ya Waislamu katika miji mbalimbali ya Marekani.
0 comments