KIMATAIFA
KUFUATIA VIKWAZO VYA MAREKANI KWA IRAN, IRAN YASEMA ITATUMIA NJIA MUAFAKA
Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema hatua isiyo ya kisheria ya Marekani ya kujumuisha majina ya shakhsia na taasisi mpya za Iran na zisizo za Iran kwenye orodha ya vikwazo vyake haramu vya nje ya mipaka haiwiyani na ahadi ilizotoa Washington na inakinzana na kusudio la muhtawa wa azimio nambari 2331 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Taarifa hiyo ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesisitiza kuwa kuimarisha Iran uwezo wake wa makombora, ambao unafanyika kwa malengo ya kiulinzi tu na kwa ajili ya kubebea silaha za kwaida na kutumika katika kujilinda na kujihami kisheria ni haki ya wananchi wa Iran kulingana na sharia za kimataifa na Hati ya Umoj wa Mataifa.Taarifa hiyo imeeleza bayana kuwa uingiliaji wowote wa watu wengine katika suala hilo ni ukiukaji wa sharia za kimataifa na uko nje ya ustahiki wa nchi na taasisi yoyote ile.Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itachukua hatua mkabala na mwafaka dhidi ya hatua yoyote inayolenga maslahi ya wananchi wa Iran.Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesisitiza kwamba kama ambavyo katika kukabiliana na hatua ya serikali ya Marekani iliyo dhidi ya Uislamu ya kuwazuia raia wa Iran kuingia nchini humo hatua mkabala imechukuliwa kuhusiana na raia wa Marekani, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itachukua hatua pia dhidi ya uamuzi mpya uliotangazwa na serikali ya Washington.Katika muendelezo wa miamala ya kiadui ya serikali ya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Wizara ya Fedha ya nchi hiyo jana ilitoa taarifa ya kuwajumuisha shakhsia 25 wa kawaida na wa kinyadhifa kwenye orodha ya vikwazo dhidi ya Iran.Vikwazo hivyo vipya vilivyowekwa na Marekani kwa kisingizio cha jaribio la kombora lililofanywa na Iran vinakinzana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na vilevile azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa…/
Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema hatua isiyo ya kisheria ya Marekani ya kujumuisha majina ya shakhsia na taasisi mpya za Iran na zisizo za Iran kwenye orodha ya vikwazo vyake haramu vya nje ya mipaka haiwiyani na ahadi ilizotoa Washington na inakinzana na kusudio la muhtawa wa azimio nambari 2331 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Taarifa hiyo ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesisitiza kuwa kuimarisha Iran uwezo wake wa makombora, ambao unafanyika kwa malengo ya kiulinzi tu na kwa ajili ya kubebea silaha za kwaida na kutumika katika kujilinda na kujihami kisheria ni haki ya wananchi wa Iran kulingana na sharia za kimataifa na Hati ya Umoj wa Mataifa.
Taarifa hiyo imeeleza bayana kuwa uingiliaji wowote wa watu wengine katika suala hilo ni ukiukaji wa sharia za kimataifa na uko nje ya ustahiki wa nchi na taasisi yoyote ile.
Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itachukua hatua mkabala na mwafaka dhidi ya hatua yoyote inayolenga maslahi ya wananchi wa Iran.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesisitiza kwamba kama ambavyo katika kukabiliana na hatua ya serikali ya Marekani iliyo dhidi ya Uislamu ya kuwazuia raia wa Iran kuingia nchini humo hatua mkabala imechukuliwa kuhusiana na raia wa Marekani, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itachukua hatua pia dhidi ya uamuzi mpya uliotangazwa na serikali ya Washington.
Katika muendelezo wa miamala ya kiadui ya serikali ya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Wizara ya Fedha ya nchi hiyo jana ilitoa taarifa ya kuwajumuisha shakhsia 25 wa kawaida na wa kinyadhifa kwenye orodha ya vikwazo dhidi ya Iran.
Vikwazo hivyo vipya vilivyowekwa na Marekani kwa kisingizio cha jaribio la kombora lililofanywa na Iran vinakinzana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na vilevile azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa…/
0 comments