DONALD TRUMP ATETA JAMBO NA NETANYAHU
HakiEPAImageRais Donald Trump wa Marekani akipeana mkono wa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wakati wa mkutano na waandishi habari, nchini Marekani
Rais Trump amemkaribisha waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika ikulu ya Marekani, na kusema atafanya kazi kwa bidii kwa kile alichokiita makubaliano ya amani kati ya Israel na Palestine.
Amesema pande zote mbili zitahitajika kuwa na maridhiamo, na kwamba angetaka Israel isitishe kidogo ujenzi wa makazi unaoendelea.
Kwa upande wake, bwana Netanyahu amesema Israel sharti ihakikishe kuwepo kwa usalama katika eneo la linalokaliwa la West Bank.
Amesema hivi sasa kuna fursa kubwa ya kuwepo kwa makubaliano ya amani kwa kushirika wajumbe wengine wa nchi za kiarabu.
Bwana Netanyahu pia amesema anaamini kwamba uongozi wa bwana Trump unatoa fursa ya kihistoria ya kubadilisha kile alichokiita kama kuwepo kwa wimbi la waislamu wenye msimamo mkali.
Source: BBC swahili
0 comments