SABABU ZA WOLPER KUTOA POVU KWA WANAOMNANGA ZARI
UKITAJA majina makubwa ya wasanii wa filamu za Bongo Movies, huwezi kuliacha jina la Jackline Wolper Massawe, mwanadada ambaye amecheza muvi nyingi za kusisimua na kuelimisha.
Akiwa kama mgeni mualikwa wikiendi iliyopita kwenye sherehe ya 40 ya motto Nillan wa Diamond pale Madale, Wolper alifunguka maneno mazito sambamba na kuwaponda ambao wanamchafua mpenzi wa Diamond, Zari kupitia mitandao ya kijamii. Global TV Online ndiyo ilikuwa ya kwanza kuiachia hewani video hiyo ambayo bado ina-trendi mpaka sasa.
Akiwa mgeni mualikwa kwa mara nyingine tena, jana usiku kwenye hafla ya Irene Uwoya Valentines’ Party iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Next Door, Masaki, Wolper alipata fursa ya kufunguka kupitia Global TV Online akielezea sababu za kuwashambulia wanaomchafua Zari.
“Siyo kwamba nilikuwa nimelewa, no! Nilikuwa naongea kutoka moyoni, mimi ni kioo cha jamii kwa hiyo nina kila sababu ya kuzungumza ukweli ninapoona baya linatendeka.
“Watu wengine wakiona wewe ni kioo cha jamii, wnataka unyamaze usiseme hata kama unaona kuna maovu, mimi huwa napenda kusema ukweli, na nitaendelea kusema ukweli tu siku zote.” Alisema Wolper.
0 comments