Pacha waliotenganishwa Kenya watembezwa nje ya hospitali
HakiKENYATTA NATIONAL HOSPITAL
Pacha waliozaliwa wakiwa wameshikana sehemu ya chini ya mgongo lakini wakatenganishwa na madaktari hospitali kuu ya taifa ya Kenyatta, Nairobi Novemba mwaka jana, walifanya matembezi yao ya kwanza jana nje ya hospitali hiyo.
Watoto hao Blessing na Favor walitembezwa katika kituo cha wanyamapori cha Animal Orphanage, Nairobi kuwaona wanyama Siku ya Wapendanao.
Ilikuwa mara yao ya kwanza kutoka hospitalini tangu walipolazwa 5 Septemba, 2014.
Pacha hao walifanyiwa upasuaji wa kuwatenganisha, ambao ulitajwa na wengi kuwa ufanisi mkubwa wa madaktari Kenyatta, tarehe 2 Novemba mwaka jana.
Afisa mkuu mtendaji wa hospitali hiyo Lily Koros Tare alisema acha hao wamepiga hatua sana tangu wafanyiwe upasuaji.
HakiKENYATTA NATIONAL HOSPITALImageWakiondoka hospitaliniHakiKENYATTA NATIONAL HOSPITALImageWakijionea simbaHakiKENYATTA NATIONAL HOSPITAL
Chanzo: BBC swahili
0 comments