Warembo waliojipanga na bikini
Serikali Guinea imepiga marufuku kwa muda maonyesho ya urembo baada ya mavazi ya bikini kuzua shutuma nchini humo.
Wagombea walijipanga mbele ya waziri mkuu Mamady Youla wakiwa wamevaa bikini siku ya Jumamosa na kasababisha shutuma kwenye mitandao ya kijamii.
Gazeti moja liliandika likiuliza ikiwa waziri mkuu alikuwa akiunga mkono ukahaba.
Waziri wa tamaduni anasema kuwa marufuku hiyo itasalia hadi pale vipengee vipya vya maadili vitatangazwa.
Amasema kuwa kamati imebuniwa kuandika vipengele hivyo.
Pia amesema kuwa serikali imefuta mikataba na waandalizi wa maonyesho hayo ya urembo.
Chanzo: BBC
0 comments