Popular Posts
-
Uvaaji wa cheni au shanga kiononi kwa wanawake ni aina ya utamaduni ambao umekuwa ukipendwa sana na wanawake hasa wa pwani tangu miongo ming...
-
Kumekuwa na tabia au hali ya wanawake wengi kupiga kelele au unaweza kusema kutoa sauti wakati wakishiriki tendo la ndoa. Hali hii imeacha m...
-
Miaka ya hivi karibuni kua na makalio makubwa imekua ni fasheni muhimu sana kiasi kwamba wanawake wasio na makalio makubwa wamejikuta wakipa...
Powered by Blogger.
Social Counter
My Blog List
Comments
Social Share
Recent in Sports
.
..
KITAIFA
ABDUL NONDO AICHAMBUA SIRI ILIYOPO UTATA WA KAMPUNI YA MINJINGU MINES NA COUNTY BUNGOMA
February 28, 2017 ibra 2 CommentsMbunge wa serikali ya wanafunzi CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM 'Abdul NONDO' ametoa maoni yake kuhusu MINJINGU MINES AND FERTILIZER LTD VS BUNGOMA COUNTY GOVERNMENT FERTILIZERS kama ifuatavyo..
'Sasa hivi kila mtu anajiuliza kwanini Mbolea ya minijingu inayozalishwa na minjingu mines and fertilizers LTD, iliyopo TANZANIA na huzalisha mbolea hiyo kwa kutumia malighafi kutoka kwetu TANZANIA ambayo ni madini ya phosphates yaliyopo manyara (mgodi)
Lakini Jambo la kushangaza hapa ni vifungashio hivyo kuandikwa BUNGOMA COUNTY GOVERNMENT FERTILIZERS Nairobi kenya.
Hadi sasa Hakuna anaye fahamu kwanini wamefanya hivyo, lakini director wa minijingu Hans Tosky anasema kuwa wa wateja wao ndio wanapenda kuona vifungoshio vya namna hiyo. ambayo ni sababu ambayo haipo wazi kwanini.
BUNGOMA COUNTY ni mji uliopo Kenya mpakani wa Uganda upande wa magharibi wa Kenya (kaunti ya bungoma) huu mji una serekali ambayo ni jimbo kiongozi huwa ni governor hii ni kwa sababu Kenya bunge lao ni BICAMERAL, mji wa bungoma unajishuhulisha saana na kilimo, biashara, na hata viwanda vya miwa. hadi sasa haijulikani kwa nini MBOLEA YA TANZANIA IANDIKWE Bungoma government county fertilizers ingawa uchunguzi unafanyika lakini yafuatayo yanawezekana ya kawa ni sababu ya haya.
Kenya kumukuwa na kampeni kubwa ya kutoa ya punguzo nafuu kwa wakulima wake ambao hawana uwezo, na wajane wamekuwa wakipewa bure mbolea hiyo (subsidized fertilizers) ,na serekali ya BUNGOMA imekuwa mstari wa mbele wa kutekeleza haya, governor KEN LUSAKA amekuwa mstari wa mbele.
Kwa tatizo hili kuna uwezokano mkubwa kumefanyika CONTRACTING MANUFACTURING,(uzalishaji wa mkataba),huu ni aina ya mkataba ambao unaingiwa Kati ya Kampuni na mzalishaji (hiring firm and manufacturer) kuzalisha bidhaa kwaniaba ya kampuni hiyo kwa kwa makubaliano ya bei ambapo msambazaji na mtafuta soko ni kampuni hiyo.
hapa kuna uwezekano mkubwa Kenya kuna kampuni au hata serekali ya Bungoma kuwa imeingia makubaliano na mkataba na Minijingu mine and fertilizer Ltd kuwa kama mzalishaji yaani manufacturer wa kwa makubaliano yao ya bei, na hiyo kampuni ya bungoma county au hata serekali ya bungoma kuwa msambazaji mkubwa wa mbolea hiyo, kwa kupokea tenders mbali mbali.kwa sababu tuu serekali ya Kenya imekuwa ktk kampeni kubwa ya kugawa mbolea kwa wakulima na ndio maana wananchi wa manyara wamekuwa wakilalamika na hata Waziri Mkuu alisema kuwa wananchi hao hawauziwi hiyo mbolea badala yake wanaagiza nje, hii ni kwasababu anazalisha kwa ajili ya kampuni fulani,kwa ajili ya watu fulani.
Katika mkataba huwa makubaliano yanaweza kuwa minijingu mine and fertilizer limited chini ya TOSKY HANS aandike jina jina hilo.
mambo mengi yanaweza husika humo mfano ukwepaji wa kodi(export tax) , soko, ndio maana kuna uchunguzi lakini haya yanawezekana kabisa Na Kama wakibainika na shutuma yeyote wachukuliwe hatua kali ili kukomesha tabia hiyo sababu hatutaweza kujitangaza kimataifa na tukasifika,pia hatutaweza kuwa na soko.
Pia tunakosa kodi (export tax), ambayo Kenya ndio wanayoipata sababu order zote huishia Kenya.
Shukrani'
Abdul Omar Nondo .
0659366125
KIMATAIFA
UTAFITI: UGANDA NDIO NCHI YA KWANZA KUONGEA KIINGEREZA FASAHA BARANI AFRIKA
February 28, 2017 ibra 0 CommentsUganda imetajwa kuwa nchi yenye raia wanaozungumza lugha ya Kiingereza kwa ufasaha barani Afrika.
Utafiti uliofanywa na shirika la lugha duniani World Linguistic Society umesema Uganda inaongoza ikifuatiwa na Zambia halafu Afrika Kusini ikiwa katika nafasi ya tatu na Kenya katika nafasi nne.
Uganda imetajwa kuwa nchi yenye raia wanaozungumza lugha ya Kiingereza kwa ufasaha zaidi barani Afrika
Kulingana na gazeti la The New Vison nchini Uganda, utafiti huo unajiri kufuatia kanda ya video iliomuonyesha malkia wa urembo kutoka Rwanda akishindwa kujielezea kiingereza.
The New Vison linasema kuwa mwaka 2015, mmoja wa malkia hao wa Urembo katika shindano la Malkia wa urembo nchini Rwanda Uwase Honorine alishindwa kujibu maswali aliyoulizwa na majaji wa shindano hilo.
Rwanda iliokuwa chini ya koloni ya Ufaransa ilianza kuzungumza Kiingereza baada ya kukosana na Ufaransa.
Gazeti la The New Vision linasema kuwa kiingereza nchini Uganda ndio lugha rasmi, na ndio lugha inayotumiwa katika shule na taasisi tofauti nchini humo.
Watoto huanza kujifunza lugha hiyo katika shule za msingi.
The New Vison linasema kuwa hivi majuzi serikali iliziagiza shule kufunza lugha za nyumbani kwa wale wanaosoma katika shule za msingi lakini ikasisitizia kuwa Kiingereza ndio lugha itakayotumiwa katika mtaala.
Mataifa yanayozungumza kiingereza kwa ufasaha:
1.Uganda
2. Zambia
3. South Africa
4 . Kenya
5. Zimbabwe
6. Malawi
7. Ghana
8. Botswana
9. Sudan
KIMATAIFA
BREAKING: BARACK OBAMA KUGOMBEA URAIS WA UFARANSA TENA ?
February 28, 2017 ibra 0 CommentsOmbi la mtandao la kumtaka Barrack Obama kuwania urais katika uchaguzi mkuu nchini Ufaransa limewavutia takriban wafuasi 42,000.
Mabango ya kampeni yanayosomeka ''Oui, on Peut'' ikimaanisha kauli mbiu ya kmpeni ya Obama ''Yes we can'' yametumika mjini Paris.
Bwana Obama sio raia wa Ufaransa hivyobasi hawezi kugombea urais.
Lakini wale wanaofanya mzaha huo wanasema kuwa lengo lao ni kuonyesha kwamba hakuna wagombea wazuri .
Ujumbe wao kwa wagombea hao kama alivyosema mmoja ya waandalizi wa ombi hilo ni ''jamani hamufai'.
Mabango yalio na picha ya Obama yamewekwa mjini Paris
Wapiga kura wa Ufaransa watashiriki katika uchaguzi mkuu mnamo tarehe 25 mwezi Aprili na iwapo wagombea hawatapata asilimia 50 ya kura katika raundi ya kwanza basi wapiga kura watarudi tena mnamo tarehe 7 mwezi Mei ili kuamua kati ya wagombea wawili waliopata kura nyingi.
Mgombea mwenye umaarufu katika uchaguzi huo ni Marine Le Pen ambaye amenufaiki na shutuma zinazomkabili mpinzani wake Francois Fillon tangu mwezi Januari hatua iliomfanya hakimu mmoja kusema kuwa ataanzisha uchunguzi kuhusu madai hayo.
Kura mbili za maoni zinamuonyesha Marine Le pen akiongeza dhidi ya Fillion lakini inasemekana kwamba wapinzani wake wanaweza kumshinda iwapo itafikia awamu ya pili ya uchaguzi
Rais wa Marekani Donald Trump amesema anaamini kuwa Barack Obama ndiye anahusika na maandamano dhidi ya uongozi wa Republican.
"Nafikiri Rais Obama anahusika kwa sababu ni watu wake wanaohusika kwenye maandamanohayo," Trump alikiambia kituo cha Fox News.
Trump hakutoa ushahidi wowote kwa madai yake na Obama bado hajajibu lolote.
Trump pia alizungumzia bajeti na masuala mengine.
Alipoulizwa kuhusu maandamano yanayohusu amri ya kusaka. alisema kuwa ni wafuasi wa Obama waliohusika.
KITAIFA
NEWS: MTANDAO WA WANAFUNZI WAKAMILISHA KUJINOA KUPINGA MALIPO YA 15% YA MKOPO MAHAKAMANI
February 28, 2017 ibra 0 CommentsTAARIFA KUTOKA KWA LHRC na TSNP
LHRC na TSNP tumekutana leo kujadili suala la malipo ya 15% kwa watanzania waliokopeshwa na bodi ya mikopo.
Tumefanya majumuisho ya hoja za kisheria kwa wajumbe waliofika kikaoni na wale ambao wamewasilisha maoni yao kwa njia ya simu, barua pepe na jumbe za kawaida kutoka kila kona ya Tanzania. Njia ya kushinda dhahama hii ni pana sana.
Muhimu zaidi, tunashukuru tumepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wanafunzi na kutoka kwa vyama mbalimbali vya wafanyakazi wanaokiri kuonja uchungu mzigo huo mzito. Wengi wanasema wako tayari kulipa 8% kama sehemu ya deni lao ila sio 15% kwani ni kiwango kikubwa sana.
Hata hivyo, matamanio yetu ni kuona vyama vingine vya wafanyakazi nchini vinachukua hatua ya kuunga juhudi hizi kama ambavyo TUCTA wamefanya hii leo.
Wanachama wao wanatoa sehemu ya misharaha yao kwajili ya mambo kama haya yanayogusa maisha yao moja kwa moja, sio kwajili ya viongozi na watumishi wengine kujilipa mishahara na posho.
Pamoja na dalili zote kuonesha ushindi, imani yetu kama taasisi (TSNP) ni kupambana kukataa mzigo huu(15%) mzito mpaka tuone ushindi. Tutashinda. 15% haikubaliki.
©Bob Wangwe
-Mkurugenzi wa sheria TSNP
BURUDANI
MAPOKEZI YA AIRPORT: ALI KIBA 'MFALME RASMI' WA BONGO FLAVA atua na tuzo ya MTV EMA
February 28, 2017 ibra 0 CommentsMashabiki wa muimbaji Alikiba wamejitokeza kwa wingi JK Nyerere Airport kumpokea mkali huyo wa Aje akitokea Afrika Kusini huku akiwa na tuzo yake na MTV EMA – Best African Act.
Akiwa Afrika Kusini alifanya media tour pamoja na show katika kumbi mbalimbali nchini huyo.
Muimbaji huyo aliiwambia waandishi wa habari kuwa tour yake hiyo ilikuwa na mafanikio makubwa katika muziki wake.Angalia picha na video za tukio hilo.
Akiwa Afrika Kusini alifanya media tour pamoja na show katika kumbi mbalimbali nchini huyo.
Muimbaji huyo aliiwambia waandishi wa habari kuwa tour yake hiyo ilikuwa na mafanikio makubwa katika muziki wake.Angalia picha na video za tukio hilo.
BURUDANI
MAKAVU: T.I.D ''MNYAMA'' >> STEVE NYERERE NI ''PANYA'' TU KWANGU
February 28, 2017 ibra 0 CommentsHivi karibuni, kwenye mazungumzo yaliyovuja kati yake na mama yake na Wema Sepetu, alidai kuwa hitmaker wa Siamini, TID alipewa fedha na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,
Mnyama alimind mbaya na kutishia kumshtaki mchekeshaji huyo. Na sasa mkali huyo ameibuka na kumwelezea Steve kuwa si staa kwake, bali ni kama panya tu.
“Steve Nyerere sio staa kwangu, he is a mouse,” ameiambia E-News ya EATV.
“Ukimuangalia kwanza he is a mouse, to me, me I have been doing this talent na nimejijengea umaarufu kupitia kipaji changu, sio kupitia uongo uongo, udananda sijui umbea umbea, sijafanya hivyo,” ameongeza.
“I have been working very hard to make this name. Huwezi kuniambia mimi eti nimepewa milioni mbili sijui, unanidhalilisha, kwanza unanihatarishia maisha yangu mtaani mimi nionekane snitch, nimewasnitch wananchi, nimepewa milioni 3 kuconfess pale, why? Milioni mbili na maisha yangu?
TID amemtaka Steve afike mbele ya mahakama athibitishe kuwa alichukua shilingi milioni 2, lasivyo patachimbika.
BURUDANI
Nicki Minaj amtaka Trey Songz akanushe tetesi kuwa waliwahi kulala pamoja…
February 28, 2017 ibra 0 Comments- Baada ya rapa Remy Ma kutoa diss kali kwa Nicki Minaj na kutaja majina ya mastaa tofauti, wengi wao wameanza kujitetea kuhusu tuhuma zao kwenye diss hio.
Nicki alichotaka Trey afanye ni kusema JAMBO HILO HALIJAWAHI KUTOKEA na sio kujibu kwa mafumbo ili kuendeleza stori hio….
Trey Songz anatajwa kwenye SHETHER kama mwanaume aliyewahi kuwa na mahusiano na Nicki Minaj na kwamba walilala pamoja mara moja tu >> “Only time you touched a Trigga was when you fucked Trey Songz / Coke head, you cheated on your man with Ebro.”<<
Trey anasema “I got respect for Nicki. Me and Nicki did work together,I got respect for Remy. But no matter what you heard, I ain’t never had sex with Nicki.”
Na kwenye twtter ameandika >>“Even when you stay out of the way they will have ya name all in some shit. Wake up to new comedy everyday. Focus,”
Jibu hili halikumridhisha Nicki Minaj ambaye kwenye twitter naye ameandika “Lol, Wut u SHOULD b saying is that it’s not true, seeing as it’s not. Real ni**az do real things. I done gotchu 6 million plaques.”