BURUDANI
Wema Sepetu au Batuli? Tumuamini yupi kati yao
Wiki chache zilizopita kumekuwepo na mambo mengi ambayo yamekuwa yakitrend kwenye vichwa vya watu kama madawa ya kulevya, watu kupelekwa kuhojiwa na harakati za wanahabari kutaka kujua msanii gani atapanda mahakamani, lengo ni kutaka kuchukua matukio mbalimbali yatakayotokea maeneo hayo.
Ukiacha na hayo, kumekuwa na habari ambayo msanii wa Filamu Tanzania, Wema Sepetu kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Hatua hiyo ilizua mshangao kwa baadhi ya watu kwasababu Wema alikuwa ni kada mahiri wa chama cha Mapinduzi, CCM. Nikisema hivyo simaanishi alivyokuwa CCM asingeweza kuhama chama hicho lahasha, bali ni uhuru wa kidemokrasia tulionao Watanzania mtu kuhamia chama unachokipenda bila kubugudhiwa na mtu.
Safari ya Wema na Freeman Mbowe Mahakama Kuu ya Tanzania
Kabla ya kujitangaza rasmi, Wema aliongozana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe katika mahakama kuu ya Tanzania ambapo aliwapa sintofahamu watu waliopo katika mahakama hiyo kwa kunyoosha vidole viwili juu.
Kumbuka hapo Wema alikuwa hajatangaza kujiunga rasmi na chama hicho, ila aliongozana tu na viongozi hao. Siku iliyofuata Wema na mama yake (Mariam Sepetu) waliita waandishi wa habari nyumbani kwao Sinza Mori na kutangaza rasmi kuikimbia CCM na kuhamia Chadema na kuanza kujiita kamanda.
Safari ya Wema na waandishi wa habari
Wema alipoita waandishi hao kulikuwa na baadhi ya nukuu ambazo watu walizisikia akizizungumza, moja ya kauli hizo ni kwamba ‘Kipindi cha kampeni 2015 hawakulipwa na CCM, kwa maana hiyo anakidai chama hicho pesa za kampeni. Pia alidai alivyoamua kujiunga CHADEMA, hajapewa hata shilingi kumi akidai kuwa amejiunga nacho wa mapenzi yake mwenyewe.
Batuli na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Hoteli ya Protea
Siku kadhaa baada ya Wema kusema anaidai CCM, waliokuwa naye kwenye kampeni hizo za Mama Ongea na Mwanao akiwemo Yobnesh Yussuf maarufu kama Batuli, walipinga kauli yake.
Batuli alisema kuwa Wema ni muongo na kudai kiwa wote walilipwa na lengo la maneno hayo ni kumchafua makamu wa Rais huku wakidai kuwa hawatahama katika chama hicho. Waliongeza kuwa kama Wema ameamua kuhama, ahame kimya kimya na si kukichafua chama chao (CCM)..
Hii ni nukuu ya Batuli, “Nikiwa kama makamu mwenyekiti wa group hili la Mama Ongea na Mwanao kwa muda ni kweli inasemekana kwenye mitandao kuwa tulifanya kampeni na hatukulipwa, mimi kama mwenyekiti msaidizi wa muda nakanusha taarifa hizo kuwa si za kweli.
Ingawa kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani,wapo wanaoshawishiwa kulichafua kundi letu, kumchafua Makamu wa Rais Bi Samia Suluhu na kuichafua CCM, mimi nakataa, sote tumelipwa na mikataba ipo, haiwezekani we staa mkubwa unakaa kwenye media unaongea uongo kwamba wasanii hatujalipwa.”
0 comments