Breaking News
Loading...

Morogoro: Walimu wakuu wa shule zilizofanya vibaya darasa la saba wakabidhiwa vinyago vyao

Share on Google Plus


Walimu wakuu wa shule za msingi Magunga na Lubanta, Wilaya ya Mvomero zilizofanya vibaya kwenye mtihani wa darasa la saba mwaka jana, wamekabidhiwa kinyago.


Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mohamed Utaly alikabidhi kinyago hicho katika tukio lililoshuhudiwa na walimu wakuu wa shule za msingi na waratibu elimu kata wa wilaya hiyo, shule hizo zitakaa na kinyago hicho kwa kupokezana ndani ya miezi sita kila shule.

Shule zilizofanya vizuri zimepatiwa vyeti maalumu vilivyosainiwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako ili ziongeza bidii.

Ofisa Elimu ya Msingi wilayani Mvomero, Michael Ligola alisema kutokana na wilaya hiyo kufanya vibaya kitaaluma katika matokeo ya mwaka jana, walifanya utafiti mdogo wa kuzunguka kwa baadhi ya kata kuona kilichosababisha hali hiyo.

Ligola alisema asilimia 80 ya matatizo waliyoyabaini katika maeneo mengi uwezo wake upo ndani ya maeneo husika, ikiwamo kuwahusisha wakuu wa shule na waratibu.

Source: Mwananchi

You Might Also Like

0 comments

About me

Like us on Facebook

MICHEZO

Blog Archive