Breaking News
Loading...

Wanajeshi kumi wa Mali wauawa na wavamizi wenye silaha

Share on Google Plus

Duru za kijeshi za Mali zimaerifu kuwa wanajeshi wasiopungua kumi wa jeshi la nchi hiyo wameuawa na watu waliokuwa na silaha.


Duru moja ya jeshi la Mali imeeleza kuwa wanajeshi hao kumi wa jeshi la Mali waliuawa jana na watu wenye silaha katika kituo cha kijeshi karibu na eneo la Boulikessi katika mpaka wa nchi hiyo na Burkina Faso.

Maeneo ya kaskazini na katikati mwa Mali ambayo yameathiriwa na machafuko

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wavamizi hao wameiba pia silaha nyingi katika uvamizi huo. Mali ambayo ni moja ya nchi za Magharibi mwa Afrika mwaka 2012 ilitumbukia katika hali ya mchafukoge baada ya kujiri mapinduzi na sasa nchi hiyo inakabiliwa na upinzani wa makundi mbalimbali yanayobeba silaha.


 Serikali na wapinzani huko Mali walisaini makubaliano ya amani mwaka 2015 lengo likiwa ni kuhitimisha machafuko katika maeneo ya kaskazini na katikati mwa nchi, hata hivyo maeneo hayo yangali yanashuhudia mapigano ya makundi yenye silaha.

Kikosi cha kudumisha amani cha Umoja wa Mataifa na wanajeshi wa Ufaransa wako huko Mali tangu katikati ya mwaka 2013, hata hivyo wameshindwa kurejesha amani ya kudumu nchini humo.

   

You Might Also Like

0 comments

About me

Like us on Facebook

MICHEZO

Blog Archive