KIMATAIFA
Korea kaskazini yarusha makombora Japan
Jeshi la Korea kusini limesema Korea kaskazini imerusha makombora yake kadhaa katika bahari ya Japan, Jeshi la Korea kusini limesema kuwa makombora hayo yamerushwa kutoka kwenye eneo la Tongchang-ri lililo kwenye mpaka kati ya Korea kaskazini na China na kurushwa kwa umbali takriban kilomita elfu moja.
Maeneo ambayo makombora yalirushwa
Akiongea na waandishi wa habari, waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema makombora hayo yanadhihirisha ushaidi tosha wa vitisho vipya kutoka kwa Korea kaskazini
''Korea kaskazini imefyatua makombora yake manne leo na kuangukia karibu na eneo letu la maji lenye manufaa kwetu kiuchumi.
Japan itakusanya taarifa na kuzichambua kuhusu tukio hili.Japan inaipinga vikali Korea kaskazini.makombora yaliyorushwa wakati huu inaonyesha wazi kuwa Korea kaskazini ni tishio jipya.Korea kaskazini ilishatangaza aina hii mpya ya makombora kabla ya kuyarusha leo hivyo, tutafuatilia kwa karibu suala hili kwa kwa umakini mkubwa''.
0 comments