KITAIFA
Lissu akamatwa na Polisi Mahakamani Kisutu Dar
Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, amekamatwa na Jeshi la Polisi katika maeneo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam.
Lissu amekamatwa Jumatatu hii asubuhi. Alienda mahakamani hapo kusikiliza kesi yake nyingine ya uchochezi na kukamatwa nje ya mahakama hiyo mara baada ya kumaliza kusikilizwa kwa kesi hiyo.
Global Publishers ilifanikiwa kuzungumza na Ofisa Habari wa Chadema Tumaini Makene, ambaye amethibitishwa kukamatwa kwa Lissu.
“Ni kweli Tundu Lissu amekamatwa alipokuwa akitoka mahakamani kusikiliza kesi yake. Polisi hawajaeleza kwanini wamemkamata na huenda wamempeleka kwa Kamanda Simon Sirro kuhojiwa, hatuna taarifa zaidi tutawajuza,” alisema Makene.
0 comments