KITAIFA
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres kuwasili Nchini usiku huu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres anatarajiwa kuwasili Nchini usiku huu wa saa 4 akitokea Kenya.
Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa atafanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Agustino Mahiga kisha kuondoka zake hapa nchini.
Waziri Mahiga atamuwakilisha Rais John Pombe Magufuli ambaye yupo Mkoani Dodoma kikazi.
Source: Azam News
0 comments