BURUDANI
Kala Jeremiah simjui, ndio nani? – Dayna Nyange NINI KINAENDELEA?
Nini kinaendelea kati ya Dayna Nyange na rapper Kala Jeremiah, kwani muimbaji huyo wa Komela amedai hamjui rapper huyo wa wimbo Wanandoto.
Wiki hii muimbaji huyo akizungumza na mtangazaji wa Enewz ya EATV, alikataa kuzungumzia ishu za rapper huyo huku akidai kwamba hamjui.
“Ukifanya interview na mimi usiniulizie habari za huyo mtu, simjui mbona mnapenda kumpa mtu kiki. Ndio nani Kala Jeremiah,” alisema Dayna Nyange.
Baada ya kauli hiyo Bongo5 ilimtafuta rapper huyo na kuzungumza naye kuhusiana na kauli hiyo ambayo imeibua maswali mengi kwa mashabiki wa muziki.
“Dayna Nyange ni mshikaji wangu, sio mpenzi wangu ana mtu wake na mimi na mtu wangu, sina ugomvi naye na huwa naongea naye kwenye simu, sema akiulizwa swali hilo sijui kwa nini anasema hivyo, ni uwamuzi wake lakini mimi sina tatizo naye na wala siwezi kumwongelea kwa mabaya,” alisema Kala
0 comments