BURUDANI
MBWA MWENYE MDOMO WA AJABU AOLEWA MAREKANI.
Mbwa aliyetelekezwa na mmiliki wake kwa kuwa na mdomo ulio kombo ameokolewa.
Mbwa huyo kwa jina Picasso aliokolewa pamoja na nduguye Pablo mjini Oregon nchini Marekani.
Wawili hao walitupwa katika jumba moja la wanyama baada ya mmiliki wao kushindwa kuwauza.
Walichukuliwa na mfugaji mwengine wa mbwa ambaye huwaokoa mbwa wanaotelekezwa.
Kulingana na miliki wake Picasso, alizaliwa akiwa na tatizo hilo la uso .
Licha ya kutupwa Picasso mwenye umri wa miezi 10 anafuraha.
Alitarajiwa kufugwa pekee na mmiliki wake mpya lakini ikagundulia kwamba alikuwa na ndugu ambaye pia angetelekezwa.
”Hatukuweza kumwacha nduguye ,kwa hivyo tukaamua kwamba pia tumchukue”, ilisema kampuni hiyo ya uokoaji wa mbwa katika mtandao wake wa Instagram
0 comments