KIMATAIFA
Watu wanne wauawa mapiganoni Kongo
picha hii haina uhusiano na tukio |
Watu wanne wameuawa katika mapigano kati ya polisi na kundi moja linaloipinga serikali huko Kinshasa mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Celestin Kanyama Inspekta wa polisi ya Kinshasa ameashiria kuawa polisi mmoja na wanachama watatu wa kundi moja linaloipinga serikali na kueleza kuwa, askari polisi wamemtia mbaroni Ne Muanda Nsemi mjumbe wa kundi hilo la upinzani linaloipinga serikali ya Kinshasa.
Insepekta wa polisi ya Kongo ameongeza kuwa wamenasa na kukamata silaha na idadi kubwa ya zana za kijeshi. Celestin Kanyama amesema kuwa mjumbe huyo wa kundi hilo la upinzani aliyetiwa mbaroni atahukumiwa kwa mujibu wa sheria.
Ne Muanda Nsemi, Mjumbe wa kundi linaloipinga serikali ya Kinshasa aliyetiwa mbaroni
Inspekta wa polisi ya Kongo ameongeza kusema kuwa Ne Muanda Nsemi anatuhumiwa kumdhalilisha Rais Joseph Kabila wa Kongo na kuchochea machafuko na uasi nchini.
Kushindwa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuyaangamiza makundi ya wanamgambo nchini humo, kumesababisha kuenea hali ya mchafukoge na ukosefu wa amani nchini humo.
0 comments