KITAIFA
Watu Watatu wamekufa na wengine 28 kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyohusisha basi la Ilyana mkoani Njombe .
Watu Watatu wamekufa na wengine 28 kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyohusisha basi la Ilyana mkoani Njombe .
Basi hilo lenye namba T 202 Dgk lilikuwa likifanya safari zake kutoka jijini dsm ,kwenda mkoani Ruvuma, ambapo waliofariki katika ajali hiyo ni wanaume Wawili na mwanamke Mmoja.
Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Pudensiana Protas amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika eneo la Image kata ya Igominyi baada ya basi hilo kupinduka majira ya saa mbili usiku wa jana.
Kamanda Protas amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa gari hilo ambapo ametoa wito kwa abiria kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama mara dereva anapoendesha gari kwa mwendokasi ili kuepusha ajali.
Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Njombe huku majeruhi wa ajali hiyo wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.
SOURCE: TBC
0 comments