MICHEZO
MESSI AWEKA REKODI MPYA UINGEREZA
Lioneil Messi bado tu anaonekana mpinzani wa karibu wa Crstiano Ronaldo.Kila wawili hawa wakicheza wanaonekana kuweka rekodi mpya.Wakati wa mechi ya juzi kati ya Barcelona dhidi ya Sportin Gijon Lioneil Messi aliweka rekodi mpya ambayo mwanzo ilikuwa ikishikiliwa na Roberto Carlos.
Messi ameweka rekodi ya kuwa mchezaji kutoka nje ya Hispania kucheza michezo mingi katika ligi kuu ya Hispania La Liga.Mess amefikisha michezo 371.Kabla ya mchezo huo Messi alikuwa michezo sawa na mlinzi wa zamani wa Real Madrid Roberto Carlos wakiwa wamecheza michezo 370.Hii ni orodha ya wachezaji wanaotoka nje ya Hispania waliocheza mechi nyingi La Liga.
Lioneil Messi.(371).Messi raia wa Argentina mshindi mara 5 wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia,kwa sasa Messi ndiye anayeshikilia rekodi hii ya mchezaji kutoka nje ya Hispania kuwahi kushiriki katika mechi nyingi La Liga.
Roberto Carlos 1996 – 2007 (370).Raia mwingine anayetokea Amerika ya Kusink.Roberto Carlos mmoja kati ya walinzi bora kabisa wa kushoto kuwahi kutokea anashika nafasi ya pili.Carlos aliwasili Real Madrid kutoka Inter Millan na kucheza mpaka mwaka 2007 alipotimkia Fernabache.
Mauro Silva 1996 – 2005(369).Mauro ameshawahi kushinda kombe la dunia akiwa na Brazil mwaka 1994.Mauro alipowasili Deportivo hadi anaondoka mwaka 2005 alifanikiwa kushinda kombe la Copa del Rey mara mbili na Spanish super cup mara 3.
Duda 2001 – hadi sasa(312).Duda raia wa Ureno aliwasili La Liga mwaka 2001 akiichezea Malaga.Baadae Duda alijiunga na klabu ya Sevilla,Duda anakumbukwa haswa baada ya kumpiga Xabi Alonso kiwiko.
Mauricio Pochettino 1995-200 na 2004-2006(275).Kwa sasa ni kocha wa Tottenham Hotspur,Pochettino ndiye aliisaidia Espanyol kupanda La Liga.Pochettino alikuwepo katika kikosi kilichochukua ubingwa wa kwanza ndani ya miaka 60 Espanyol,ilikuwa mwaka 2000 walipochukua Copa del Rey.Baadae Pochettino alihamia Psg lakini akarudi tena baada ya miaka 6 na kuchukua Copa Del Rey
0 comments