Wakimbizi 50 wameuawa katika shambulizi la bahati mbaya nchini NIGERIA
Kikosi cha Jeshi la anga cha nchini NIGERIA kimeua kwa bahati mbaya zaidi ya wakimbizi 50 na wafanyakazi wa kutoa msaada wakati wa operesheni dhidi ya wanamgambo wa kundi la BOKO HARAM.
Shambulio hilo la bahati mbaya limesababisha vifo vya baadhi ya wakimbizi na wafanyakazi wa Shirika la kutoa Msaada, MSF |
Kikosi cha Jeshi la anga cha nchini NIGERIA kimeua kwa bahati mbaya zaidi ya wakimbizi 50 na wafanyakazi wa kutoa msaada wakati wa operesheni dhidi ya wanamgambo wa kundi la BOKO HARAM.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la kutoa misaada MSF, Dkt JEAN-CLEMENT CABROL amesema zaidi ya wakimbizi 120 wamejeruhiwa huku wafanyakazi sita wa shirika lake wakiuawa kutokana na shambulizi hilo.
Dkt CABROL amesema Shambulio hilo limetokea karibu na mpaka wa nchni Cameroon ambapo amewataka askari wa kulinda amani kuheshimu haki za binadamu wakati wa operasheni zao za kijeshi.
Msemaji wa rais nchi NIGERIA amesema serikali imesikitishwa kwa tukio hilo, na kuomba radhi kwa wahanga wote na kueleza kuwa NIGERIA itatoa msaada wa kutosha kwa majeruhi na waathirika wote.
1 comments
Endelea kutujuza kwa habari zuri nafurahia habari zako
ReplyDelete