AZAM FC YAPATA PIGO, YAPOTEZA KIONGOZI WAKE
November 7 2016 taifa la Tanzania limepata pigo kwa kupokea taarifa za kifo cha mbunge wa zamani wa Urambo na Spika wa bunge wa zamani mzee Samuel Sitta, baada ya taarifa hizo kuenea zimeripotiwa taarifa nyingine za klabu ya Azam FCkumpoteza aliyekuwa mwenyekiti wao Said Mohamed.
Mzee Said Mohamed amefariki November 7 2016 akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Agakhan Dar es Salaam, mzee Said alikuwa na mchango mkubwa katika soka sio tu ndani ya klabu yake ya Azam FC.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri mzee Said Mohamed alikuwa meneja mkuu wa makampuni ya SSB, mwenyekiti wa Azam FC, makamo mwenyekiti wa bodi ya Ligi na mjumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho la soka Tanzania TFF.
0 comments